Storm FM

Paka wa ajabu aleta taharuki kwa kufanya shambulio.

3 January 2023, 9:02 am

Na Kale Chongela:

Watu watatu akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka (5) wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na paka wa ajabu majira ya alfajiri katika Kitongoji cha kilimahewa Kata ya Lulembela wilayani  mbogwe Mkoani Geita.

Tukio hilo limezua taharuki kwa wakazi wa mtaa huo huku baadhi ya mashuhuda akiwemo mama mzazi wa mtoto huyo wamesema, paka huyo alitokea kusikojulikana kisha kuanza kuwashambulia na kujeruhi watu watatu akiwemo  mtoto.

Mwenyekiti wa mtaa wa kilimahewa Katendele Busumabu amekiri kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake huku akiwaomba wananchi kutolihusisha na Imani za kishirikina.