Storm FM

Wahujumu miradi Geita kukiona cha moto

19 February 2024, 12:11 am

Kamati ya siasa Mkoa wa Geita ikiwa katika jengo la Halmashauri ya Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick

Kushindwa kukamilika kwa wakati miradi ya maendeleo Mkoani Geita imebainika kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanafanya hujuma.

Na Mrisho Sadick:

Serikali Mkoani Geita imeagizwa kuwachukulia hatua kali watu wanaohujumu na kuchelewesha miradi ya maendeleo kwasababu zao binafsi licha ya serikali kutoa fedha kwa wakati.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila akizungumza baada ya kukagua mradi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila akiwa na Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale ambapo hapo awali ujenzi wake ulianza kwa kusuasua.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema ujenzi wa Jengo hilo hadi kukamilika utagharimu zaidi ya Bilioni mbili huku Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame akimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha nyingi za Utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale