Storm FM

Maonesho ya sita ya madini Geita, kusisitiza uhifadhi wa mazingira

3 September 2023, 11:00 am

Picha ya maonesho ya tano ya uwekezaji katika sekta ya madini katika viwanja vya EPZ kata ya Bombambili, Geita. Picha na Storm FM

Maonesho ya sita ya Madini yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu mkoani Geita, yanatajwa kuwa chachu ya kuufungua mkoa kiuchumi na kuongeza fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya Madini.

Na Said Sindo -Geita

Bwana Charles Chacha kutoka Idara ya Uwekezaji, viwanda na biashara kutoka ofisi ya mkoa wa Geita wakati akizungumza na Storm FM ofisini kwake leo Septemba 03, 2023 amesema, Maonesho hayo ni fursa kwa wazalishaji, watafiti, na waongezaji thamani ya madini ambao watakutana katika maonesho hayo watakaofika kujifunza na kuangalia fursa za uwekezaji.

Sauti ya Bw. Charles Chacha kutoka Idara ya uwekezaji, viwanda na biashara kutoka ofisi ya mkoa wa Geita

Katika hatua nyingine, Bwana Chacha amesema lengo la Maonesho haya ni kuwaleta pamoja wachimbaji wadogo, wachimbaji wa kati na wakubwa waweze kukutana kwa pamoja na kubadilishana ujuzi na utaalam ili wananchi waweze kujifunza mbinu mpya za kutafiti madini ili wasichimbe kwa mazoea.

Sauti ya Bw. Charles Chacha kutoka Idara ya uwekezaji, viwanda na biashara kutoka ofisi ya mkoa wa Geita

Maonesho ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yalianzishwa mwaka 2018 ambapo katika maonesho ya mwaka jana kulikuwa na washiriki 302, lakini mwaku huu maonesho hayo yanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 600 wa ndani na nje ya Tanzania.

Maonesho haya ya sita ya kitaifa ya teknolojia ya Madini 2023 yamebeba kauli mbiu isemayo “Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira”.