Storm FM

Wachimbaji Dhahabu wakubali kukatwa 2% ya mauzo

11 July 2023, 10:32 am

Wachimbaji wadogo na wauzaji wa Dhahabu Geita wakiwasikiliza maafisa wa TRA. Picha na Mrisho Sadick

Kutokuwepo kwa mfumo rasmi wa utunzaji wa kumbukumbu za manunuzi na mauzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu hali ambayo ilikuwa ikichangia wengi wao kukwepa kodi, serikali imefanya mabadiliko ya sheria ili kila mchimbaji aweze kulipa kodi.

Na Mrisho Sadick:

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mkoani Geita wamekubali kukatwa asilimia mbili ya mauzo ya madini hayo kwenye masoko ya dhahabu ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko ya sheria mpya ya kodi ambayo imeanza kutumika mwezi huu.

Wakizungumzia mabadiliko hayo katika kikao kilichoandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Geita kwa ajili ya kuwakumbusha utekelezaji wa sheria hiyo ambayo imeanza kutumika mwezi huu,  baadhi ya wachimbaji na wanunuzi wa dhahabu Asia Masimba, Nassoro Juma na John Luhemeja wamesema wako tayari kuilipa huku wakiiomba serikali kuendelea kupunguza utiriri wa kodi katika sekta hiyo.

Wachimbaji wadogo na wauzaji wa Dhahabu Geita wakiwasikiliza maafisa wa TRA. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya wachimbaji na wanunuzi wa Dhahabu

Afisa wa kodi Mkoa wa Geita Sadick Kassim amesema walengwa katika kodi hiyo ni wachimbaji wadogo wenye leseni na ambao hawana leseni huku lengo likiwa nikuboresha mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwakuwa hapo awali kulikuwa na changamoto ya ukwepaji wa kodi.

Afisa wa Kodi Geita Sadick Kassim akitoa elimu kwa wachimbaji wa dhahabu. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Afisa wa Kodi Mkoa wa Geita Sadick Kassim