Storm FM

Auziwa mtungi wenye unga wa muhogo kwa ndani

16 July 2023, 1:17 pm

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto  na Uokoaji mkoani Geita Inspekta Edward Lukuba. Picha na Mrisho Sadick

Matukio ya utapeli katika nyanja mbalimbali yamekithiri ikiwamo katika upande wa upatikanaji wa vifaa vya kuzimia moto na uokoaji, jambo lililomuinua Inspekta Lukuba kuzungumzia hilo.

Na Kale Chongela- Geita

Jeshi la zimamoto na ukoaji mkoni Geita limewataka wananchi kufika katika ofisi za zimamoto pindi wanapohitaji kununua vifaa vya kuzimia moto ili kuepukana na vishoka.

Sauti ya Inspekta Edward Lukuba

Wito huo umetolewa na Kaimu kamanda wa Jeshi la zimamoto  na Uokoaji Mkoani Geita Inspekta Edward Lukuba  akiwa ofisini kwake ambapo amesema pamekuwepo na matepeli ambao wamekuwa wakiwauzia wananchi vifaa vya kuzimia  moto vyenye unga wa mhogo kwa ndani.

Sauti ya Inspekta Edward Lukuba

Aidha Inspekta Lukuba amesema wapo mawakala ambao wamependekezwa na Jeshi hilo kwa ajili ya kuuza vifaa vya kuzima moto huku akiwataahadharisha wananchi kuepuka matepeli.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi mjini Geita wamesema endapo elimu itazidi kutolewa mara kwa mara itasaidia kwa haraka kufahamu namna ya kutambua kifaa bora cha kuzima moto, sambamba na namna ya kutumia kifaa hicho pindi moto unapotokea.