Storm FM
Storm FM
26 June 2026, 2:34 pm

Kampuni ya GGML imeendelea kuimarisha mahusiano na Jamii pamoja na serikali kwa kufadhili miradi mbalimbali ya CSR ambayo imetajwa kuendelea kuchagiza maendeleo ya mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujuma.
Na: Ester Mabula
Kampuni ya Geita Gold Minning Limited (GGML) inayojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini mkoani Geita imetoa ufadhili wa shilingi milioni 251 ili kufanikisha mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwa wajasiriamali katika halmashauri ya wilaya ya Geita.
Akizungumza Juni 25, 2026 Afisa mwandamizi wa miradi ya CSR kutoka GGML, Masaki Godlove akiwa katika katika hafla ya kushuhudia awamu ya kwanza ya mavuno ya samaki kutoka kikundi cha Jiendeleze mchangani kilichopo katika kata ya Nkome amesema waliwezesha kikundi hicho cha wajasiriamali kiitwacho Jiendeleze mchangani kwa kuwapatia vizimba vinne, vifaranga vya samaki 120,000 pamoja na tani 36 za vyakula.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Geita Karia Rajabu Magaro ametoa pongezi kwa kikundi hicho kilichoanza mradi huo mwezi Disemba, 2025 pamoja na kuishukuru GGML kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali akieleza kuwa dhamira ya serikali ni kuendelea kushirikiana na wawekezaji kutoa fursa.

Baadhi ya wanakikundi cha Jiendeleze Mchangani wameeleza kuwa mradi huo umesaidia katika kubadili maisha yao sambamba na kujiongezea kipato huku wakiishukuru GGML kwa kuwawezesha.
