Storm FM

Mama arudishwa kwao kisa kajifungua mtoto mwenye matatizo

14 April 2021, 6:36 pm

Na  Joel Maduka:

Mwanaume anaejulikana kwa jina la LEORNARD MFI mwenye (24) mkazi wa Kata ya Kaseme Wilayani Geita anadaiwa kumrudisha mke wake nyumbani kwao kwa sababu ya kujifungua mtoto mwenye ugonjwa wa kichwa kujaa maji.

Mtoto huyo mwenye umri wa miezi mitano aliyepewa jina la ELIZABETH LEORNARD anasumbuliwa na tatizo hilo tangu kuzaliwa kwake , mama mzazi BI ZAWADI JUMA amesema alipomshirikisha mume wake katika hilo amekuwa ni mgumu katika kutoa gharama za matibabu ya mtoto wao.

Mama wa Mtoto

Bi Zawadi amesema mwanzoni mume wake alikubali kumhudumia mtoto huyo lakini ushauri mbaya kutoka kwa baadhi ya ndugu zake ulisababisha mumewe kubadili mawazo nakuacha kuwahudumia.