Storm FM

Wakuu wa idara wazembe Chato kuchukuliwa hatua

4 July 2023, 11:02 am

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na baraza maalumu la kujadili taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Halmashauri ya wilaya ya Chato. Picha na Mrisho Sadick.

Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wamekuwa na kasumba ya kutohudhuria vikao vya baraza la madiwani jambo ambalo limemsukuma Mkuu wa Mkoa kutoa maagizo.

Na Zubeda Handrish -Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa wakuu wa idara wa Halmashauri ya wilaya ya Chato ambao wamekuwa hawahudhurii vikao vya baraza la madiwani.

Shigela amesema hayo baada ya kukuta wakuu wa idara wawili ndio wamehudhuria katika baraza maalumu la kujadili taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela.

Mkoa wa Geita kuwachukulia hatua za kinidhamu wakuu wa idara

Taarifa ya ofisi ya taifa ya ukaguzi wilaya ya Chato imewasilishwa na mwakilishi mkaguzi mkuu wa nje wa hesabu za serikali Lutengano Humbo huku mwenyekiti wa halmashauri ya chato Batholomeo Manunga akikerwa na utendaji mbovu kwa baadhi ya watumishi.