Storm FM

Wakamatwa kwa kumfanyia ukatili mtoto

9 July 2023, 5:48 pm

Wananchi walioandamana katika tukio la mtoto kufanyiwa ukatili. Picha na Said Sindo

Matukio ya ukatili yamekuwa yakiendelea katika maeneo mbalimbali nchini, licha ya juhudi binafsi ya jamii kwa kushirikiana na serikali kuendelea kukemea na kuwachukulia hatua kali wanaofanya vitendo hivyo.

Na Said Sindo- Geita

Baadhi ya akina mama mtaa wa Ibolelo maarufu Mwabasabi uliopo kata ya Nyankumbu wilayani na mkoani Geita, wameandamana na kukusanyika katika nyumba ya bwana Robison wakishinikiza kuchukuliwa hatua baba na binti yake ambao wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kumnyima chakula na kumnyanyasa kwa kumchoma moto mdomoni na kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kijana Bina Robison mwenye umri wa miaka mitano.

Akina mama hao wakiongozwa na mabalozi wa mashina ya mtaa huo wamesema unyama huo wa kusikitisha umefanyika muda wote huo licha ya kuripotiwa kwa Afisa Mtendaji wa mtaa huo Mei 20 mwaka huu na baba yake mzazi akiendelea na maisha kama kawaida.

Sauti za wananchi katika mtaa wa Ibolelo wakizungumzia tukio la ukatili.

Hata hivyo majirani hao wanakiri kwamba wamekuwa wakimuona mtoto huyo akikohoa na kulia hasa nyakati za usiku, lakini walikuwa na wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina au ana matatizo ya akili.

Sauti za wananchi katika mtaa wa Ibolelo wakiendelea kuzungumzia tukio la ukatili.

Marafiki wa mtoto huyo aliyefanyiwa vitendo vya ukatili nao wamezungumzia hali ilivyokuwa.

Sauti za Marafiki wa mtoto huyo aliyefanyiwa vitendo katika mtaa wa Ibolelo

Mtuhumiwa huyo akiwa chini ya ulinzi wa wananchi akijibu maswali aliyoulizwa huku akibabaika amesema kukonda na kudhoofika kwa mtoto huyo kumetokana na mabadiliko ya hali ya hewa tu.

Sauti ya Anastazia Robson, mtuhumiwa wa tukio la ukatili kwa mtoto wa miaka 5

Hali ya mtoto huyo imesababisha mashuhuda waliokuwa wamezunguka nyumba hiyo, kuanza kumshambulia Binti huyo  na kumlazimu Kamanda mkuu wa Polisi jamii Nzereli Nyarukama na Mwenyekiti wa mtaa huo Stephano Samson Magidinga kufanya kazi ya ziada kumnusuru mtuhumiwa kwa kumpeleka kituo cha polisi huku wakijaribu kuzuia asidhurike.

Sauti ya Kamanda mkuu wa Polisi jamii Nzereli Nyarukama
Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa huo Stephano Samson Magidinga

Afisa ustawi wa jamii halmashauri ya mji wa Geita Bw. Cathbeth Byabato amewashukuru wananchi kwa hatua walizozichukua za kunusuru maisha ya mtoto huyo huku akisema kuwa wataangalia njia nzuri ya kumsaidia endapo watatakiwa kufanya hivyo.