Storm FM

Wanawake tujishughulishe na kazi kuepuka utegemezi

27 May 2021, 2:22 pm

Wanawake katika kata ya Mgusu wilayani Geita wameshauriwa kujishughulisha na biashara ndogo ndogo za halali ili kuepuka utegemezi katika jamii.

Hadija Said – Mchimbaji wa madin ya Dhahabu

Rai hiyo imetolewa na wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa uchimbaji wa madini ya dhahabu wa mgusu miners wakati wakizungumza na Storm FM nakusema kuwa licha ya kufanya kazi za uchimbaji wa madini ya dhahabu wamelazimika kuanzisha biashara ndogo ndogo.

Katika hatua nyingine wanawake hao wamesema, kwasasa wanawake wanapewa nafasi katika maeneo mbalimbali tofauti na miaka ya nyuma, nakutumia fursa hiyo kuwashauri wanawake wengine kuendelea kupambana ili kujikwamua kiuchumi.

Makamu Mwenyekiti wa mgodi wa mgusu Miners Bi Pendo Matata amesema wanawake wengi wanaendelea kujitokeza katika mgodi huo kufanyabiashara mbalimbali huku wengine wakijihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu.