Storm FM

Maporomoko ya tope Geita yaacha kilio kwa wakulima

18 April 2024, 4:51 pm

Muonekano wa baadhi ya mashamba ya wakazi wa Nshinde yaliyovamiwa na udongo. Picha na Mrisho Sadick

Licha ya mvua kuwa ni neema lakini imegeuka kuwa kilio kwa wananchi wengi mkoani Geita kutokana na mvua hiyo kuacha simanzi kila inaponyesha.

Na Mrisho Sadick – Geita

Zaidi ya Ekari sita za mashamba ya mazao ya chakula na biashara katika mtaa wa Nshinde Kata ya Nyankumbu wilayani Geita  yameharibiwa na maporomoko ya udogo ambayo yametokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Mkoani Geita.

Tukio hili nimuendelezo wa matukio kadhaa ambayo yametokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Geita huku wahanga wa tukio hilo wakisema mazao yaliyofunikwa na udongo ni pamoja na mpunga, mahidi , viazi vitamu, mihogo na miti.

Sauti ya wahanga wa tukio
Muonekano wa baadhi ya mashamba ya wakazi wa Nshinde yaliyovamiwa na udongo. Picha na Mrisho Sadick

Inadaiwa kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka 1998 katika eneo hilo huku Mjiolojia kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGML Mussa Kasano amesema chanzo cha  maporomoko hayo ni maji kuzidi kwenye ardhi iliyoshindwa kuyahimili.

Sauti ya mjiolojia na mkurugenzi mji wa Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amewaondoa hofu wananchi kuwa hakuna mlipuko wowote ambao umejitokeza nakuiagiza halmashauri ya mji kuhakikisha inafanya tathimini ya uharibifu huo hara.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita
Muonekano wa baadhi ya mashamba ya wakazi wa Nshinde yaliyovamiwa na udongo. Picha na Mrisho Sadick

Itakumbukwa januari 30 mwaka huu wilayani chato mkoani Geita yalitokea maporomoko ya udongo kama haya ambayo chanzo chake kinafanana na tukio hili ambapo baadhi ya nyumba ziliharibiwa na mazao kusombwa na maji.