Storm FM

Vitendo vya ulawiti watoto tishio Geita

17 May 2024, 9:32 am

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita SACP Safia Jongo akizungumza na wakazi wa kata ya shabaka. Picha na Mrisho Sadick

Vitendo vya ukatili kwa watoto Geita ikiwemo ulawiti vimeendelea kushika kasi huku mamlaka zikiombwa kuendelea kuchukua hatua kali ili kuvikomesha.

Na Mrisho Sadick – Geita

Jeshi la polisi mkoani Geita limetoa tahadhari juu ya ongezeko la vitendo vya ulawiti kwa watoto huku likitoa wito kwa wazazi na walezi kujenga tabia ya kuwakagua watoto wao mara kwa mara.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi Safia Jongo wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Shabaka wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita.

Wakazi wa kata ya Shabaka wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kamanda Jongo amesema vitendo vya ulawiti kwa watoto wadogo vinazidi kuongezeka kila kukicha mkoani Geita huku vikihusishwa na imani za kishirikina nakuwataka wazazi na walazi kuwalinda watoto wao  kwakuwafanyia ukaguzi wakati wote.

Sauti ya kamanda wa Polisi Geita
Mkuu wa wilaya ya Nyan’ghwale Grace Kingalame akizungumza na wakazi wa kata ya Shabaka. Picha na Mrisho Sadick

Sanjari na hayo mkuu wa wilaya ya Nyag’hwale Bi Grace Kingalame amepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wakazi wa Kata ya shabaka kujihusisha na kilimo cha bangi huku akiahidi kuwasaka nakuwakamata.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Nyang’hwale