Storm FM

Wafanyabiashara waomba mpangilio Mzuri wa soko

19 April 2021, 6:23 pm

Na Elizabeth Obadia:

Wafanyabiashara wa wa soko la asubuhi la Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita wameuomba uongozi wa mtaa huo kuweka mpangilio mzuri wa soko ili kuwasaidia wao kupata wateja kwa wepesi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara hao wamedai kukosekana kwa mpangilio mzuri wa soko kunachangia wao kukosa wateja na kupelekea biashara zao kuwa ngumu.

Wafanyabiashara

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Bw. Mgeta Mtaki amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuwataka wafanyabiashara kuwa na uvumilivu kwani soko linatarajiwa kufanyiwa marekebisho.