Storm FM

TAKUKURU yaagizwa kumchunguza mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita

29 October 2023, 8:21 pm

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe akiwa katika kikao cha baraza la madiwani Halmasgauri ya mji wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Geita limeonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita.

Na Mrisho Sadick – Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe ameiagiza taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Geita kuchunguza safari za mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita Zahra Michuzi kama zina tija kwa Halmashauri hiyo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita kulalamikiwa kutoonekana kwenye vikao muhimu na badala yake kukaimisha maofisa wanaoshindwa kutoa majibu stahiki.

Magembe ametoa maagizo hayo katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita ambapo alihoji sababu za kutokuwepo mkurugenzi wa halmashari na kufahamishwa yupo nchini China.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe
Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Geita wakiwa katika kikao cha baraza. Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita Costantine Morandi amekiri kupokea ushauri wa mkuu wa wilaya na kuahidi kufanyia kazi kwa maslahi ya halmashauri na kufikia adhima ya maendeleo endelevu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita