Storm FM

TANESCO yaagizwa kuweka umeme shuleni

20 February 2024, 12:10 am

Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita ikiwa katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Bugegere Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia hasa katika elimu umeme umekuwa lulu kwakuwa vifaa vingi vya kufundishia vinahitaji nishati hiyo.

Na Mrisho Sadick:

Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Geita limeagizwa kufikisha umeme katika Shule ya Sekondari Bugegere wilayani Mbogwe Mkoani Geita kutokana na uwepo wa maabara za kisasa ambazo zinategemea nishati hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila ametoa agizo hilo kwa TANESCO baada ya Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita kutembelea nakukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita Joachim Ruweta akaahidi kufikia mwezi wan ne atakuwa amefikisha umeme katika shule hiyo huku mkuu wa Shule hiyo Seleman Mayala akisema imejengwa kwa thamani ya zaidi ya milioni 590.

Sauti ya meneja TANESCO na Mkuu wa shule

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed amewataka wanafunzi wa shule hiyo kutoa taarifa za wazazi wanaowazuia kwenda shule huku wajumbe wa kamati ya siasa wakawasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita ikiwa katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Bugegere Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mkuu wa wilaya na wajumbe wa kamati ya siasa