Storm FM

Wakazi wa Nyantorotoro B mjini Geita bado hawana umeme

12 June 2024, 11:02 am

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mtaa. Picha na Kale Chongela

Baadhi ya maeneo ya mtaa wa Nyantorotoro B kata ya Nyankumbu katika halmashauri ya mji wa Geita bado yana ukosefu wa umeme ambapo serikali imeanza jitihada za kupeleka nguzo katika maeneo hayo ili kuondoa changamoto ya umeme.

Na: Kale Chongela – Geita

Wakazi wa mtaa wa Nyantorotoro B kata ya Nyankumbu mjini Geita wameuomba uongozi wa serikali ya mtaa huo kutenda haki pindi unapoingia mradi wowote ili kila ubalozi uweze kunufaika na mradi husika.

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wakizungumza kwenye kikao cha dharura kilichoketi Juni 11, 2024 mbele ya diwani wa kata hiyo wameeleza baada ya  kuonekana  nguzo za umeme kutowafikia wakisema kwamba jambo hilo si la kiugwani.

Sauti ya wananchi

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Magwendela Lugololoka amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa jitihada zinaendelea kufanyika ili kila ubalozi uweze kupata nguzo za umeme kwani nguzo zilizowafikia zilikuwa ni nguzo 50.

Sauti ya mwenyekiti
Diwani wa kata ya Nyankumbu John Mapesa (aliyesimama) akizungumza na wananchi katika mkutano. Picha na Kale Chongela

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyankumbu John Lunyaba Mapesa ameeleza kuwa baada ya kukaa katika kikao hicho wameazimia kuandika barua upya ili kuanda mchoro mwingine kuruhusu kila ubalozi uweze kupata nguzo za umeme.

Sauti ya diwani