Storm FM

Wakazi wa kijiji cha Nyakayondwa hawana zahanati

9 May 2024, 3:04 am

Wakazi wa kijiji cha Nyakayondwa wakiendelea na mishe mishe za kila siku. Picha na Evance Mlyakado

Vituo vya afya na zahanati ndizo ngazi za kwanza za afya zinazoigusa jamii moja kwa moja. Licha ya serikali kuweka mpango wa kurahisisha huduma za afya kwa kuboresha miundombinu, kwa wakazi wa kijiji cha Nyakayondwa bado ni kitendawili.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Ukosefu wa zahanati katika kijiji cha Nyakayondwa kata ya Bwanga wilayani Chato umetajwa kuwa kikwazo kikubwa kwani wananchi hususani wanawake wajawazito wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Wananchi wa kijiji hicho wakizungumza na Storm fm wameiomba serikali kusaidia kukamilisha ujenzi wa majengo ya zahanati yalioanza kujengwa tangu mwaka 2017 ili wapate kupata huduma za kimatibabu.

Sauti ya wanawake
Sauti ya wanaume
Wakazi wa kijiji cha Nyakayondwa wakiendelea na mishe mishe za kila siku. Picha na Evance Mlyakado

Mwenyekiti wa kijiji hicho anakiri kuwepo kwa changamoto hiyo jambo ambalo huchangia wananchi kutumia gharama kubwa za matibabu pamoja na usumbufu kwa mama wajawazito.

Storm Fm inaendelea na jitihada za kumtafuta mkuu wa wilaya ya Chato ili kufahamu hatua zilizopo katika kuwasaidia wananchi wa kijiji cha Nyakayondwa kupata zahanati.