Storm FM

Mkoa wa Geita kupata Mahakama Kuu

13 October 2023, 1:03 pm

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akizungumza na watumishi na wadau wa Mahakama Mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Idadi ya watu milioni 2.9 katika Mkoa wa Geita imemsukuma Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia Mahakama kuu Mkoani Geita.

Na Mrisho Sadick Geita:

Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa tume ya utumishi wa Mahakama Profesa Ibrahimu Juma ameagiza kuanzishwa kwa mahakama kuu Mkoani Geita kwa lengo la kusogeza huduma za mahakama kwa wananchi.

Akizungumza na watumishi na wadau wa Mahakama Mkoani Geita katika ziara yake ya kusikiliza changamoto na michango ya jinsi gani mahakama iboreshe huduma zake amesema kuanzisha kwa Mahakama Kuu Mkoani Geita  itasaidia kuharakisha mashauri na  hukumu kutolewa kwa wakati.

Sauti ya Jaji Mkuu

Aidha Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma amewataka watumishi na wadau wa wanaoshughulika na mfumo wa haki jinai kuisoma ripoti ya tathimini iliyofanywa na taasisi ya REPOA juu ya utendaji kazi wa mahakama nchini.

Jengo la Mahakama ya hakimu mkazi Geita na mahakama ya wilaya ya Geita. Picha na Mrisho Sadick

Taasisi huru ya REPOA ilifanya Utafiti mwaka 2019 na kubaini kiwango cha utoaji haki kwa wananchi kilikuwa ni asilimia 78 lakini kwa sasa kiwango  kimepanda hadi asilimia 88 mwaka huu, huku dhana ya rushwa mahakamani ikipungua kutoka asilimia 8, 2019 hadi asilimia 6 mwaka 2023.