Storm FM

TBS yatoa mafunzo kwa wajasiriamali Geita

1 May 2021, 12:33 pm

Wajasiriamali wa  Mamlaka ya mji Mdogo  wa Katoro wilayani na Mkoani Geita  wamekutana na  viongozi wa  shirika la viwango Tanzania TBS  kwa lengo la kuwapatia   mafunzo ya kutengeneza bidha mbalimba zenye ubora na viwango vinavyokubalika.

Akizungumza kwenye  mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita  Mwalimu Fadhili Mohamed Juma  amewashauri wajasiriamali waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo kuyatumia kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Aidha Meneja wa viwango TBS Kanda ya ziwa  Mhandisi Joseph Ismaili Mwaipaja  amewataka wafanyabiashara sambamba na wajasiriamali  kuhakikisha wanauza bidha zenye ubora ambazo zimethibitishwa  na shirika la viwango Tanzania TBS .

Wakielezea kwa nyakati tofauti  baadhi ya wajasiriamali ambao wameshiriki mafunzo hayo  wameipongeza serikali kwa kuendelea kuwapatia mafunzo ambayo yamekuwa msaada kwa upande wao.