Storm FM

Wananchi wacharuka kuuziwa nguzo za umeme

15 July 2023, 6:51 pm

Picha na nyandindi2006.blogspot.com

Ukubwa wa gharama za umeme katika maeneo mbalimbali ya vijijini ni moja ya changamoto inayowanyima fursa wananchi kupata huduma ya umeme.

Na Nicolaus Lyankando- Geita

Wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini katika halimashauri ya wilaya ya mbogwe mkoani Geita wamelalamikia gharama kubwa wanazotozwa kufikishiwa huduma ya Umeme nakudai kuna mianya ya rusha hufanyika katika zoezi hilo.

Wakizungumzia changamoto hiyo baadhi ya wananchi wilayani mbogwe wamesema gharama za kufikiwa na huduma hiyo kwa sasa ni kubwa nawao imekuwa vigumu kuimudu gharama hiyo huku wakisema wamekuwa wakitozwa mpaka gharama za kulipia nguzo jambo ambalo limewatia mashaka huenda kunauonevu kwa wananchi wenye hali ya chini.

Picha na nyandindi2006.blogspot.com
Sauti ya wananchi wanaoishi kijijini halimashauri ya wilaya ya mbogwe

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Nyikonga moja ya vijiji vilivyofikiwa na huduma hiyo
Mperwa Sekela amekiri kukumbana na kesi za mara kwa mara kwa wananchi juu ya gharama
hizo nakuiomba serikali isikie kilio cha wananchi hao.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Nyikonga Mperwa Sekela

Akitolea majibu ya malalamiko Hayo meneja wa shirika la Umeme TANESCO wilani humo
Fabian Lukiko kwanza ameanza kwa kukanusha nakusema hakuna gharama anayotoa
mwananchi kwajili ya nguzo ya umeme.

Sauti ya meneja wa TANESCO Mbogwe Fabian Lukiko

Halimashauri ya wilaya ya Mbogwe ina zaidi ya vijiji 83 na zaidi ya nusu ya vijiji hivyo
imeshafikiwa na huduma ya umeme.