Storm FM

Ujuzi wa mama yake wamtoa kimaisha.

6 January 2023, 8:57 am

Na Zubeda Handrish:

Kijana Benjamin Samweli mzaliwa wa Mwanza mkazi wa Geita amezungumzia namna ambavyo mama yake mzazi amesaidia kwa kiasi kikubwa yeye kuingia kwenye biashara ya kutengeneza Culture.

Kuanza kwa kumsaidia mama yeke kutengeneza hadi kufungua ofisi yake binafsi na bidhaa mbalimbali za shanga na mavazi ya asili amesema ni hatua kubwa katika maisha yake na shukrani ni kwa familia yake kwa kumuunga mkono.

Benjamin amewaasa vijana kutochagua kazi kwani amesema pia amekutana na changamoto nyingi za wateja na ameweza kuzikabili huku baadhi ya watu wakiamini kuwa kazi anayofanya ni ya kike.

Ujuzi huo alioupata kutoka kwa mama yake ndio unaoendesha maisha yake, pamoja na kumsaidia kupata aseti mbalimbali yeye kama kijana na anapenda anachokifanya.

Je, wewe kijana ujuzi wako uliupata kutoka wapi?