Storm FM

Manga yapata mifuko 100 ya saruji kuendeleza ujenzi wa Zahanati

4 September 2023, 10:46 am

Wananchi wa mtaa wa Manga kata ya Mgusu, wilayani na mkoani Geita

Ukosefu wa Zahanati katika mtaa wa Manga kwa takribani miaka zaidi ya 10 kumewaibua wananchi na viongozi wa serikali ya mtaa huo.

Na Zubeda Handrish- Geita

Wakazi wa mtaa wa Manga kata ya Mgusu wilayani na mkoani Geita, wamefunguka adha ya muda mrefu wanayopitia ya ukosefu wa zahanati katika eneo lao na kutumia zahanati jirani ya Nyakabale ambapo kufika ni umbali mrefu wa takribani kilomita 4.

Nuru imeanza kuonekana katika mtaa huo wa Manga baada ya wananchi hao kuanzisha ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao wenyewe kwa kushirikiana na serikali ya mtaa.

Sauti ya wakazi wa mtaa wa Manga

Afisa Mtendaji na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Manga nao wamezungumzia adha zilizokuwepo, hamasa ya wananchi kuanzisha zahanati na msaada wa muwekezaji katika eneo lao.

Sauti ya Afisa Mtendaji na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Manga
Wakazi wa mtaa wa Manga wakishusha mifuko ya saruji 100 walipewa na muwekezaji wa mtaa huo Bw. John Luhende

Muwekezaji John Luhende ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Resourcess na mmiliki wa mgodi wa Nyamatagata amefunguka kilichomsukuma kuwasaidia wananchi hao wa Manga, kwa kuwachangia mifuko 100 ya saruji ili kujenga jengo la watoa huduma watakaokuja kuhudumia katika zahanati hiyo.

Sauti ya Muwekezaji John Luhende ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Resourcess na mmiliki wa mgodi wa Nyamatagata

Yapata miaka 12 tangu kuanzishwa kwa mtaa wa Manga mwaka 2014, ikiwa ni zaidi ya miaka 10 adha ya ukosefu wa huduma ya afya inawakabili wananchi wa mtaa huo.