

10 October 2024, 11:10 am
Leo ni siku ya 9 tangu kuanza kwa maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini mkoani Geita ambayo yameendelea kufanyika kila mwaka yakiwakutanisha watu mbalimbali.
Na: Ester mabula – Geita
Kampuni ya Njema Labs inayojihusisha na upimaji wa sampuli za madini amepongeza uwepo wa maonesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita kwani yanarahisisha watu kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na haraka.
Akizungumza na Storm FM Oktoba 9, 2024 akiwa katika maonesho hayo ameeleza kazi na shughuli mbalimbali wanazofanya kupitia Njema Labs.
Aidha amesema kuwa maonesho ya mwaka huu yamekuwa na mwitikio mkubwa kuliko ya miaka iliyopita na hivyo yanawasaidia zaidi katika kuendelea kuwafikia watu mbalimbali.