

10 May 2025, 1:29 pm
Wilaya ya Geita imeendelea na kampeni ya usafi wa mazingira yenye lengo la kuweka manispaa kuwa safi sambamba na kuepuka magonjwa yatokanayo na uchafu.
Na: Kale Chongela:
Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba ameipongeza redio ya Storm FM kwa kuendelea k,uhamasisha Jamii umuhimu wa kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara sambamba na makazi yao kupitia kampeni ya ‘HYAGULAGA GEITA’
Mhe. Komba amesema hayo leo Mei 10, 2025 akiwa katika mtaa wa Nyantorotoro B kata ya Nyankumbu, halmashauri ya Manispaa ya Geita baada ya zoezi la usafi lililokutanisha madereva pikipiki na kundi la wanawake na Samia mkoa wa Geita ambapo amesema Storm FM imekuwa redio bora katika kuhabarisha jamii suala la kufanya usafi wa mazingira.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyantorotoro B Bw. Juma Seif Ally ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wa mtaa huo kuhakikisha kila mmoja anafanya usafi katika eneo lake.
Katibu wa madereva pikipiki kata ya Nyankumbu Bw. Moses Baraka amesema wamelazimika kufanya usafi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya katika kampeni yake ya HYAGULAGA GEITA ikimaanisha SAFISHA/FAGIA Geita .
Afisa mazingira Manispa ya Geita Bw. Edward Mwita amesema suala la usafi ni lazima kwa kila mmoja ili kundokana na magonjwa yatokanayo na uchafu.