Storm FM
Storm FM
3 March 2026, 16:25

“Dhamira kuu ya programu hii ni pamoja na kuwawezesha watoto wa kike kufikia ndoto zao kwa kuwajengea uwezo wa kujiamini na kutokata tamaa kwenye masomo yao” – Khadija Kisatu, msimamizi wa Rasilimali watu wa GGML
Na: Ester Mabula
Programu ya uongozi na ushauri (mentorship) kwa wasichana wa shule za sekondari mkoani Geita inayoendeshwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetajwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wasichana katika shule za sekondari Nyalwanzaja na Kamena tangu ilipoanzishwa mwaka 2020.
Wakizungumza kuhusu mafanikio ya programu hiyo, walimu wa shule hizo Oscar John, Mwalimu wa shule ya sekondari Kamena na Mulebe Mfungo, Mwalimu wa shule ya sekondari Nyalwanzaja wamesema kumekuwa na mabadiliko chanya kitaaluma kwa wanafunzi wa kike sambamba na ongezeko la kiwango cha ufaulu.

Baadhi ya wanafunzi wanufaika na programu hiyo Christina Mussa, Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Nyalwanzaja na Lucia Deogratius, mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Kamena wameeleza kuwa kupitia mafunzo ya uongozi, ushauri wa kitaaluma na stadi za maisha wanazopata inawasaidia kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao kimasomo na kimaisha.

Khadija Kisatu ni Msimamizi wa Rasilimali watu kutoka GGML amesema dhamira ya program hiyo ni kusaidia jamii inayowazungukakwa kuwajengea wasichana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi huku Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto wilaya ya Geita Christina Katana akiwahimiza wanafunzi kutoa taarifa mapema pindi wanapokumbana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
