Storm FM

Nzoya na nyoka wa ajabu Geita

12 December 2025, 12:26

Shidiku akiwa na nyoka wake nyumbani kwake Mwagimagi Kata ya Nyanguku. Picha na Mrisho Sadick

Idadi ya nyoka alionao inalingana kabisa na idadi ya watoto wake tisa , Hata hivyo licha ya utaalamu alionao Shidiku anakiri kwamba kuishi na viumbe hao kunahitaji moyo wa ziada.

Na Mrisho Sadick:

Shidiku Nzoya mwenye umri wa miaka (35) Mkazi Kata ya Nyanguku Manispaa ya Geita amekuwa gumzo  kwa kucheza na Nyoka na Fisi  kama chanzo chake kikuu cha kipato ingawa kazi hiyo imewastaajabisha wengi kwakuwa viumbe hao anaishi nao nyumbani kwakwe.

Kwa Shidiku kuishi na viumbe hao si jambo la kutisha kama inavyodhaniwa na watu wengi ,amezoea kuwaona kama marafiki wa kila siku, na kupitia maonesho anayoyafanya amekuwa akipata kipato kinachowezesha kuendesha familia zake mbili zenye jumla ya watoto tisa.

Nyoka wa shidiku wakiwa nyumbani kwakwe baada ya kufikiwa na Storm FM. Picha na Mrisho Sadick

Idadi ya nyoka alionao inalingana kabisa na idadi ya watoto wake tisa , Hata hivyo licha ya utaalamu alionao Shidiku anakiri kwamba kuishi na viumbe hao kunahitaji moyo wa ziada na gharama ambazo si ndogo kwani analazimika kuhakikisha nyoka na fisi wake wanapata chakula stahiki.

Merry Nehemia ni afisa utamaduni wa Manispaa ya Geita amesema serikali inaendelea kuvipa kipaumbele vikundi vya asili huku akibainisha ni wapi vibali vyakutumia nyara za serikali vinatolewa.

Shidiku akiwa nyumbani kwake akizungumza na Storm FM. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya ripoti ya stori hii na Mrisho Sadick