Storm FM

Washiriki 400 waanza maonesho katika viwanja vya EPZA Geita

21 September 2023, 5:33 pm

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela akizungumza na wanahabari. Picha na Zubeda Handrish

Washiriki kutoka mataifa mbalimbali kama vile China, Rwanda, Burundi na mengineyo yameshiriki maonesho hayo ya 6 yaliyoanza rasmi mwaka 2018.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema kuwa maonesho ya dhahabu ambayo yameanza jana Septemba 20, 2023 katika viwanja vya EPZA mjini Geita yameanza kwa mwitikio mkubwa wa washiriki ikilinganishwa na mwaka jana.

Ameyaema hayo leo Septemba 21, 2023 katika viwanja vya EPZA na kuongeza kuwa hadi kufikia leo washiriki 400 kutoka ndani na nje ya nchi wamefika katika maonesho ikiwa ni idadi kubwa ya washiriki ukilinganisha na washiriki 250 wa mwaka jana.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela
Banda la Geita Gold Mine Limited katika viwanja vya maonesho EPZA. Picha na Zubeda Handrish

Amesema kuwa maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dr. Doto Biteko Septemba 23 mwaka huu na yatafungwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mhe. Samia Suluhu Hassan Septamba 30, mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela

Maonesho ya 6 ya kimataifa ya teknolojia ya madini 2023, yamebeba kaulimbiu isemayo “matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira”.