Storm FM

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa ndani ya tumbo la mwanamke

3 May 2024, 6:07 pm

Jopo la madaktari wakiendelea na upasuaji. Picha na Kale Chongela

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita imeendelea kupiga hatua katika utoaji wa huduma mbalimbali za kiafya ikiwemo huduma ya mama na mtoto, huduma za uchuguzi na tiba za awali za saratani ya mlango wa kizazi pamoja na huduma ya upasuaji mkubwa na mdogo.

Na: Kale Chongela – Geita

Mwanamke Evalin Paul mkazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera amefanyiwa upasuaji wa tumbo katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Geita na kuondolewa uvimbe wa kilo tano ambao amedumu nao kwa kipindi cha miaka 10.

Upasuaji huo umefanywa na madaktari bingwa wa kambi ya mama Samia waliopo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita huku mwanamke huyo akisema amehangaishwa na uvimbe huo kwa muda mrefu na akizunguka sehemu mbalimbali bila mafanikio.

Sauti ya Evelin Paulo

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka kambi hiyo Isaack Ajee amesema uzito wa uvimbe uliyokuwa katika tumbo la mwanamke huyo ni sawa na umri wa mtoto ambae amefikia muda wa kuzaliwa.

Sauti ya Dkt. Isaack Ajee
Daktari Isaack Ajee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Geita Dkt. Salum Mfaume amesema wamepokea madaktari bingwa 29 kutoka kambi ya mama Samia.

Sauti ya Dkt. Salum Mfaume
Daktari Salum Mfaume akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Wagonjwa wengine waliopatiwa huduma na kupona ni wale wenye changamoto ya kusikia kwa muda mrefu na matatizo mengine ambayo yalihitaji huduma za kibingwa.