Storm FM

Makonda azulu kaburi la JPM Chato

10 November 2023, 4:07 pm

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda. Picha na Mrisho Sadick

Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Makonda amezulu kaburi la Maguli leo hii.

Na Mrisho Sadick- Geita

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa, leo November 10, 2023 amefika nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita na kuzuru kaburi lake.

Akiwa kwenye kaburi la JPM, Makonda ameongoza sala fupi ambapo amenukuliwa akisema kuwa anamuahidi Hayati Magufuli kama anaweza kumsikia, Dkt. Samia amempa nafasi, atakuwa Msema kweli, atakuwa Mwaminifu kwa Taifa na Chama, naye huko aliko aendelee kumuombea na kwamba ile kazi njema aliyotamani ifanyike katika Taifa hili chini ya Jemedari na Kiongozi aliyemuachia atakuwa sehemu ya kumsaidia na kumtia moyo Rais Samia”.

“Pia anaamini Taifa litanufaika zaidi, na kumshukuru Hayati Magufuli kwakuwa alilipenda Taifa la Tanzania naye akaahidi kuendeleza upendo, na uzalendo na kulilinda Taifa hili na siku moja atakapotwaliwa kuacha alama kama Hayati Magufuli alivyoacha alama katika Taifa hili la Tanzania”.