Storm FM
Waumini wa dini ya kiislamu Geita washauriwa kuzidisha upenndo
14 April 2021, 5:15 pm
Na Joel Maduka:
Waislamu kote duniani leo hii wameanza kufunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo hujizuiya kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jua linapozama takriban siku 30 au 29 kutegemea na muandamo wa mwezi.
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Geita , Al haji Yusufu Kabaju amewasisitiza waislamu kuendelea kuzidisha upendo, kutoa sadaka na kuwakumbuka wote wale wenye kuhitaji msaada.
Aidha Shehe Kabaju ametaja mambo ya msingi ambayo muumini wa dini ya kiislamu anatakiwa kuyazingatia katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani.