Storm FM

Aomba kujengewa shimo la choo baada ya uharibifu mjini Geita

14 June 2024, 5:09 pm

Bi. Tumaini Ndayumbayumba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Serikali mjini Geita imeendelea na ukarabati wa barabara ambazo zimekuwa na changamoto hususani ambazo pia ziliharibiwa katika kipindi cha mvua.

Na: Kale Chongela – Geita

Bi. Tumaini Ndayumbayumba mkazi wa mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala mjini Geita ameuomba uongozi unaosimamia ujenzi wa barabara kutoka nguzo mbili hadi kwenye mtaa maarufu kwa jina la “mama Kengele” kumjengea shimo la choo ambalo limeharibiwa na gari zinazotengeneza barabara hiyo.

Shimo la choo ambalo linaelezwa kuharibiwa kutokana na utengenezaji wa barabara. Picha na Kale Chongela

Akizungumza na Storm FM Juni 13, 2024 Bi. Tumani amesema shimo la choo chake limeharibiwa na gari ambazo zinaendelea na shughuli ya ujenzi wa barabara inayojegwa kwa kiwango cha lami huku akiuomba uongozi unaosimamia mradi huo kumjengea shimo hilo.

Sauti ya Tumaini Ndayumbayumba
Shughuli za matengenezo ya barabara zikiendelea. Picha na Kale Chongela

Mshauri wa mradi huo unaotekelezwa na Benki ya Dunia TACTIC mjini Geita mhandisi Rechnold Manyanga amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kubainisha kuwa tayari wameshaanza jitihada za kumtafuta fundi ili aweze kurekebisha sehemu ambayo imeharibiwa

Sauti ya Rechnold Manyanga