Storm FM

Wanafunzi darasa la nne zaidi ya 1,000 wamefeli Nyang’hwale

17 January 2024, 11:18 am

Wadau wa elimu wakiwa kwenye kikao cha Mkakati wa kuinua elimu wilayani Nyang’hwale. Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na matokeo mabaya ya darasa la nne na kidato cha pili mwaka jana wilaya ya Nyang’hwale imeanza mikakati ya mapema ili kuepukana na changamoto hiyo mwaka huu.

Na Mrisho Sadick :

Kufuatia anguko la kufeli wanafunzi wa darasa la nne zaidi ya elfu moja 1,000 wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita Mkuu wa wilaya hiyo Grace Kingalame ameapa kuwashughulikia walimu na watendaji wa idara ya elimu wanaoishindwa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria wilayani humo.

Kingalame ametoa kauli hiyo kwenye Kikao cha tathimini na mipango ya Elimu kwa mwaka 2024 kufuatia matokeo mabaya ya Mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili huku akisema atakuwa katili kwa watendaji wa serikali watakao kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mkakati waliyojiwekea wa kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zote zilizochangia matokeo mabaya huku akiagiza wanafunzi wote waliyofeli kuhakikisha wanafuatiliwa nakurudishwa shuleni.

Grace Kingalame Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale akiwa kwenye kikao cha wadau wa elimu wilayani humo. Picha na Mrisho Sadick

Sauti ya Mkuu wa wilaya Nyang’hwale
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale katikati Husna Tony akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa Elimu. Picha na Mrisho Sadick

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Husna Tony ameahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizowasilishwa na wadau wa elimu zikiwemo za walimu kutotimiza wajibu wao ipasavyo, baadhi ya wazazi kuwashinikiza watoto kufanya vibaya na Utoro sugu.

Sauti ya Mkurugenzi Nyang’hwale na wadau wa elimu