Storm FM

Rais wa CWT ajibu mapigo baada ya kupewa siku 14 kujiuzulu

12 July 2023, 5:27 pm

Rais wa CWT Mwalimu Leah Ulaya akitolea ufafanuzi juu ya tuhuma zinazomkabili. Picha na Said Sindo

Vuguvugu na tuhuma kutoka kwa wanachama wa CWT zimekuwa kubwa kwa Rais wa chama hicho na katibu wake, suala lililopelekea Rais huyo kutoka hadharani na kujibia tuhuma zinazomkabili kutoka kwa wanachama wake.

Na Said Sindo- Geita

Ikiwa imepita wiki moja tu tangu Rais wa CWT Mwalimu Leah Ulaya na katibu wake Mwl Japhet Maganga kupewa siku 14 na chama cha walimu Mkoa wa Geita wawe wamejiuzulu kutokana na kuwepo kwa tabia ya ubadhilifu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka  amesema yote yanayosemwa ni upuuzi na wala hayana ukweli wowote huku akiwataka wananchi kuyapuuza.

Sauti ya Rais wa CWT Mwalimu Leah Ulaya akitolea ufafanuzi juu ya tuhuma zinazomkabili
Wajumbe wa chama cha walimu CWT wakijadiliana juu ya tuhuma zinazomkabili Rais wa chama hicho. Picha na Said Sindo

Leah Ulaya na katibu wake Mwl Japhet Maganga wanatuhumiwa kuendesha chama hicho kama mali yao ikiwa ni pamoja na kuitisha baraza batili la tarehe 18.06.2023 na kununua tisheti za Mei Mosi ambazo hazikufuata utaratibu wa manunuzi.

Sauti ya wajumbe wa chama cha walimu CWT wakitoa tuhuma zao kwa Rais wa chama hicho