Storm FM

Storm FM waungana na wakazi wa Mpomvu kusafisha Mazingira

4 June 2021, 9:58 pm

Wafanyakazi na viongozi wa kituo cha Storm fm kwa kushirikiana na Idara ya mazingira na wakazi wa mtaa wa Mpovu kata ya Mtakuja wamefanya usafi katika soko la mtaa huo lengo likiwa ni kuhimiza jamii kujenga desturi ya kuishi kwenye mazingira safi na salama.

Akizungumzia hatua hiyo Stesheni meneja wa Storm FM Bw Obadia Mashamba amesema lengo ni kuihimiza jamii kutambua umuhimu wa kufanya usafi.

Naye Mwenyekiti serikali ya Mtaa wa Mponvu Bw Mathias Methusela ,amesema kwa sasa wananchi wake wamekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira.

Nao baadhi ya wafanyakazi  wa storm fm,Esther Mabula na Kevin Milambo wameelezea furaha yao ya kushiriki na wananchi wa mtaa wa Mpomvu.

Maadhimisho ya siku ya mazingira dunia huadhimishwa kila June 5 ya kila mwaka na kimkoa yatafanyika wilayani chato huku yakiongozwa na Kaulimbiu ya tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ikolojia.