Storm FM

Ajeruhi Mtoto kisha kajinyonga hadi Kufa

1 May 2021, 11:40 am

Mwanaume aliejulikana kwa jina moja la Shija (30) Mkazi wa Mtaa wa Nyantorotoro “A” mjini Geita amemjeruhi Mtoto wake kwa kitu chenye ncha kali tumboni kisha na yeye kujinyonga hadi kufa huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika.

Mke wa Marehemu

Akizungumza na Storm FM katika hosptali ya mkoa wa Geita Bi Joines Bukuru ambae alikuwa mke wa marehemu amesema mume wake alimuagiza dawa dukani na aliporudi alikutana na mtoto wake akiwa nje huku anatokwa na damu alipoingia ndani alimkuta mume wake amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa.

Mke wa Marehemu

Bi Joines amesema yeye ni mzaliwa wa mkoani kigoma na Mtoto aliejeruhiwa niwa mwanaume mwingine huku akiongeza kuwa  huenda sababu ya mume wake kufanya tukio hilo ni baada ya kwenda hosptali pamoja kupimwa nayeye kugundulika na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati yeye mwanamke na mtoto wakiwa salama.

Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo wamesikitishwa na kitendo hicho huku wakisema familia hiyo imehamia katika mtaa huo hivi karibuni na walikuwa hawajafahamiana kwa undani zaidi.

Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo Bw Ng’yanya Kibigwe amekiri kuwepo kwa tukio hilo nakutumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakazi wa Mtaa huo ambao hawajajitambulisha nakuorodheshwa katika kitabu cha mtaa wafike katika ofisi yake ili kuondokana na changamoto kama iliyojitokeza kwa familia hiyo.