Storm FM

Taulo za kike za kushona mkombozi kwa familia masikini

17 August 2023, 12:35 pm

Mwanafunzi Liliani akionesha ujuzi wake wa kushona taulo za kike. Picha na Mrisho Sadick

Kundi la watoto wa kike hususani maeneo ya vijijini mkoani Geita linakatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya hedhi.

Na Mrisho Sadick:

Ujuzi wa kushona taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani Geita umekuwa mkombozi kwa familia zisizo na uwezo wa kumudu gharama za kununua taulo hizo kila mwezi.

Liliani Michael mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mwatulole mjini Geita ambaye anatoka familia ambayo haina uwezo wa kumudu gharama za kununua taulo za kike kila mwezi , amepata ujuzi wa kushona taulo hizo Kutoka shirika la Marafiki wa Elimu lenye makao yake mkoani Geita.

Sauti ya Mwanafunzi Liliani Michael

Msimamizi wa miradi wa shirika la marafiki wa elimu Amina Mvungi amesema wanafunzi wa kike wanaotoka familia duni wengi wamekatisha masomo huku wengine wakiwa watoro wanapokuwa katika kipindi cha Hedhi kwakuwa wanakosa uhuru.

Sauti ya msimamizi wa miradi Marafiki wa Elimu

Mkurugenzi wa Shirika la marafiki wa Elimu Mkoani Geita Ayobu Bwanamadi anasema wameendelea kutoa elimu katika makundi tofautitofauti ikiwemo ya wanafunzi na mtaani kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike kukabiliana na changamoto hiyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Marafiki wa Elimu
Taulo za kike za kushona zikiwa tayari kwa matumizi. Picha na Mrisho Sadick