Storm FM

Watumiaji vyombo vya moto Geita watoa maoni bei mpya za mafuta

8 August 2024, 11:58 am

Eneo la roundabout lililopo katika halmashauri ya mji wa Geita.

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) Agosti 0, 2024 imetoa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa hapa nchini zitakazotumika kwa mwezi Agosti.

Na: Ester Mabula – Geita

Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Agosti 2024 imepanda katika mikoa inayochukua mafuta hayo kwenye bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ikilinganishwa na mwezi Julai ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa inaonyesha bei za mafuta yanayochukuliwa bandari ya Dar es Salaam, petroli imepanda kwa Tsh. 21 kwa lita na kuwa Tsh. 3,231.

Katika mkoa wa Geita bei elekezi kwa kila wilaya ni kama ifuatavyo

Geita Petroli ni Tsh. 3,397 kwa lita na Dizeli ni Tsh. 3,296 kwa lita.

Chato Petroli ni Tsh. 3,418 kwa lita na Dizeli ni Tsh. 3,318 kwa lita.

Nyangh’wale Petroli ni Tsh. 3,412 kwa lita na Dizeli ni Tsh. 3,311 kwa lita.

Mbogwe Petroli ni Tsh. 3,435 kwa lita na Dizeli ni Tsh. 3,335 kwa lita.

Bukombe Petroli ni Tsh. 3,386 kwa lita na Dizeli ni Tsh. 3,285 kwa lita.

Baadhi ya watumiaji wa vyombo vya usafiri wakiwemo madereva pikipiki maarufu bodaboda pamoja na bajaj wametoa maoni yao kufuatia kutangazwa kwa bei mpya.

Sauti ya madereva