Storm FM

Wananchi wa Ilangasika watengua kauli ya kutoshiriki uchaguzi.

6 January 2023, 9:08 am

Na Said Sindo:

Baada ya kilio cha muda mrefu cha Wananchi wa Kijiji cha Ilangasika kilichopo kata ya Lwamgasa katika Jimbo la Busanda baada ya kulalamika kwa muda mrefu juu ya hai mbaya ya barabara na daraja katika kijiji hicho sasa wamepatiwa ufumbuzi.

Awali wananchi wa kijiji hicho walitishia kutojihusisha na shughuli zozote za uchaguzi utakaofanyika kwa madai kuwa wamekuwa hawatatuliwi changamoto yao ya Daraja na barabara iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Wananchi hao wamemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo la Busanda Mhe. Tumain Magesa baada ya barabara ya Busanda Buziba kuanza kutengenezwa.