Storm FM

Wezi wadaiwa kuficha mali juu ya mlima

6 May 2024, 5:32 pm

Mlima unaotumiwa na wezi kuhifadhi mali. Picha na Evance Mlyakado

Licha ya dhana ya ulinzi shirikishi na uwepo wa polisi jamii katika mitaa na vijiji vya mkoa wa Geita, bado changamoto ya vibaka na wezi imeendelea kuwatesa wakazi wa Njia panda ya Inyala katika mji mdogo wa Katoro.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Wananchi waishio jirani na mlima uliopo katika eneo la Kilimanjaro, Njia panda ya Inyala ndani ya Mamlaka ya mji mdogo wa katoro, wameonyesha kuchukizwa na vitendo na tabia ya wizi ambao unafanywa na baadhi ya watu wakiiba vitu vyao na kisha kuvitelekeza katika mlima uliopo jirani na eneo hilo.

Storm  fm imewatembelea wananchi hao na kuzungumza nao ambapo wameziomba mamlaka zinazohusika kuimarisha ulinzi kuwasaidia kuwafichua wezi hao ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.

Makazi ya watu yanayozungumka mlima. Picha na Evance Mlayakado

Balozi wa eneo hilo amekiri kupokea taarifa za malalamiko kutoka kwa wananchi na kueleza kuwa kundi la vijana ndio wanatajwa kuhusika zaidi licha ya jitihada za kuwasaka bado zinagonga mwamba.

Sauti ya balozi

Katibu wa Polisi Jamii mtaa wa Kilimahewa ametaja vitu ambavyo vimekuwa vikiibiwa na kueleza hatua ambazo wanaendelea kuchukua ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Sauti ya katibu wa polisi jamii