Storm FM

Wachimbaji watakiwa kuacha kutunza fedha kwenye mabegi

2 August 2023, 9:13 am

Kushoto Mkurugenzi TCB na kulia Mkuu wa Mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya wachimbaji wadogo wamekuwa na utamaduni wa kuweka pesa ndani, jambo linalotishia usalama wa fedha zao na fursa hiyo kutumiwa na benki ya TCB huku ikija na mpango wa mikopo nafuu kwa wachimbaji.

Serikali mkoani Geita imewataka wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu, wafanyabiashara na wajasiriamali mkoani humo kuacha utamaduni wa kutunza fedha kwenye mabegi na badala yake wazitunze kwenye taasisi za kifedha.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella wakati akizinduzi tawi la benki ya biashara nchini (TCB) katika Soko la dhahabu Geita mjini, nakusema kuwa tawi hilo ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mikakati ya kukuza uchumi wa mkoa huo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita
Kushoto Mkurugenzi TCB na kulia Mkuu wa Mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya TCB Sabasaba Moshingi amesema benki hiyo inashiriki kupambana na umasikini kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wananchi huku Meneja wa tawi hilo akieleza fursa zilizopo kwa wachimbaji.

Sauti Mkurugenzi mtendaji wa benki ya TCB na Meneja

Lakini pia wananchi wamezungumzia furaha yao kusogezewa huduma hiyo ya kibenki karibu.

Sauti za wananchi katika uzinduzi wa benki ya TCB