Storm FM

Idadi ya watalii wa ndani yaongezeka

28 June 2023, 12:42 pm

Na: Kale Chongela: Idadi ya watalii wazawa katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato imeendelea kuongezeka kutokana na hamasa inayoendelea kutolewa kwa wananchi  ikiwemo filamu ya Royal Tour ambayo imekuwa na msukumo mkubwa kwa wakazi wanaozunguka hifadhi hiyo kutembelea kujionea vivutio mbalimbali.

Hayo yamebainihswa  na Emmanuel Nyundo Askari Mhifadhi wa Burigi Chato  baada ya Baraza la  UVCCM Mkoa wa Geita kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea hifadhi hiyo huku akitaja ukubwa wa hifadhi hiyo ni kilomita za mraba 4707.  

Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mkoa WA Geita Bw  Manjale Magambo amesema wanaunga mkono Jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha Utalii wa ndani.