Storm FM

CCM yaagiza viongozi wazembe washughulikiwe Geita

24 June 2024, 7:34 am

Katibu wa NEC akiwa katikati na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akizindua ofisi ya CCM Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe Geita. Picha na Mrisho Sadick

Viongozi wazembe wanaokwamisha miradi na wenye dharau wamekalia kuti kavu mkoani Geita baada ya katibu wa NEC kuagiza wasakwe na wachukuliwe hatua.

Na Mrisho Sadick:

Katibu wa NEC Organization na mlezi wa CCM Mkoa wa Geita Issa Haji Ussi GAVU amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela kuwachukulia hatua kali viongozi wazembe wanaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akiwa katika ziara yake ya kwanza ya kutembelea nakukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa wilaya Mbogwe Mkoani Geita jana Juni 23,2024 Katibu wa NEC Organization amesema hakuna sababu ya kuendelea kuwakumbatia watendaji wazembe.

Sauti ya Katibu wa NEC Organization CCM Taifa
Wanachama na wananchi wa wilaya ya Mbogwe wakiwa kwenye mkutano wa katibu wa NEC Organization wilayani humo. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameahidi kufanyia kazi maagizo hayo huku akisema serikali imeendelea kutatua changamoto mbalimbali katika wilaya ya Mbogwe ikiwemo ya maji , afya , elimu na miundombinu ya barabara.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Geita
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na katibu wa NEC Organization wakiwa katika Ofisi ya CCM Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila amesema CCM itaendelea kuwatumia wanachama wake wenye nia ya kujitoa kukisaidia chama bila kuja maneno ya watu wenye nia ovo huku MNEC wa Mkoa wa Geita Evarist Gervas aliyesaidia ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Lugunga amesema ataendelea kukijenga chama kwa kushirikiana na wanachana wenye uchu na maendeleo.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM NA MNEC Mkoa wa Geita

Katibu wa NEC Organization akiwa wilayani Mbogwe amezindua Ofisi ya CCM ya Kata ya Lugunga iliyojengwa na wanachama kwa kushirikiana na MNEC wa Mkoa Ndugu Evarist Gervas nakutembelea shule ya sekondari ya Nyakafuru iliyojengwa kwa Gharama ya zaidi ya milioni 590.