Storm FM

Wananchi walia na waya uliopita chini kwenye makazi yao

8 December 2023, 8:53 am

Changamoto ya nyaya zilizopitishwa chini ya nyumba za watu kinyemela zimezua taharuki kwa wakazi wa Tambukareli mjini Geita.

Na Kale Chongela- Geita

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Tambukareli kata ya kalangalala mjini Geita wanaoishi pembezoni mwa Barabara ya Q Man kuelekea Lukilini wamelalamikia uwepo kwa nyaya za mawasiliano zilizopita kwenye makazi yao huku wakisema nyaya hizo zimedumu kwa muda wa miaka 3, na licha ya uwepo wa nyaya hizo wamiliki wa viwanja hawajapewa taarifa yoyote na kwamba nyaya hizo zinamilikiwa na kampuni ya Vodacom.

Wananchi Tambukareli mjini Geita wakizungumzia kero ya waya

Mhandisi wa kampuni ya Vodacom Kanda ya Ziwa Ellon Abila akizungumza kwa njia ya simu amesema eneo hilo wao ni wapangaji na kila msimu hulipa kodi.

Meneja wa wakala wa Barabara za mjini na vijijini TARURA wilaya ya Geita Mhandisi Bahati Subeya amekiri kupokea barua ya malalamiko kutoka kwa wananchi hao na kusema kuwa tayari wameshatoa maelekezo kwa kampuni hiyo kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.