Storm FM

Waziri azindua maonesho ya nne Geita.

22 September 2021, 4:29 pm

Na Mrisho Sadick:

Serikali imeahidi kusimama na wachimbaji pamoja na wafanyabiashara wa madini ya dhahabu hapa nchini kutokana na Sekta hiyo kuendelea kuongeza Pato la taifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa wakati Akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Geita kwenye hafla ya Uzinduzi wa maonesho ya teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini.