Storm FM

Waliomteka mtoto na kudai milioni 4 watiwa mbaroni Mbogwe

19 January 2024, 1:29 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo akizungumza na waandishi wa Habari . Picha na Mrisho Sadick

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limejipanga kukabiliana na matukio ya ukatili kwa watoto ikiwemo ya kubakwa na kuuawa.

Na Mrisho Shabani – Geita

Jeshi la polisi Mkoa wa Geita limewakamata watu watatu wilayani Mbogwe kwa tuhuma za kumteka mtoto mwenye umri wa miaka minneĀ  kisha watekaji hao wakaomba milioni nne ili wamwachie.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi wa polisi ACP Safia Jongo  amethibitisha kukamatwa kwa watu hao  wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na kushamiri kwa matukio ya watoto kuibiwa , kubakwa na kuuawa.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita

Katika hatua nyingine kamanda Jongo amesema Jeshi hilo limeanza msako wa waganga wanaofanya ramli chonganishi ikiwemo kuwataka wateja wao kubaka au kufanya mauaji ya watoto ili wapate utajiri.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita

Amewataka wananchi kuwa makini na watoto wao kwakuwa baadhi ya wazazi wamesahau wajibu wao wa malezi hali ambayo inaleta changamoto kubwa.