Storm FM

Kivuko cha meli Mharamba chasombwa na maji, wananchi wakwama

27 November 2023, 11:36 pm

Kivuko (Gati) cha kijiji cha Mharamba kilichosombwa na maji. Picha na Said Sindo

Mvua zinazoendelea kunyesha bado ni changamoto kwa wakazi katika maeneo tofauti mkoani hapa.

Na Said Sindo- Geita

Wakazi wa kijiji cha Mharamba, wilaya ya Geita mkoani Geita wamesema maisha yao yako hatarini kutokana na kivuko (Gati) walichokuwa wakitumia kusombwa na maji hivyo kusababisha adha ya usafiri katika eneo hilo.

Kivuko hicho hata hivyo, kimezama kutokana na maji kujaa na kusababisha wananchi hao kuvua nguo zao na wengine kubebwa mabegani ili kufanikiwa kuvuka na kwenda ng’ambo ya pili kwaajili ya kupata mahitaji yao.

Sauiti ya wananchi wa kijiji cha Mharamba, wilaya ya Geita mkoani Geita na mwenyekiti wa kijiji hicho

Awali baada ya adha hiyo kuwa kubwa kwenye eneo jirani na hilo, Mbunge wa Geita vijiji Joseph Msukuma alitoa mitumbwi kwaajili ya kuvusha wananchi wa Mharamba, Kwenda Mwembeni lakini hadi sasa wanasema imekwisha chakaa na haitoshelezi mahitaji kwani inabeba kwa wastani watu watatu tu kwa kila tripu.