Storm FM

Geita kuzalisha hekta zaidi ya laki tano za mazao ya chakula

20 November 2023, 12:24 pm

Wadau wa kilimo Mkoani Geita wakiongozwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Geita wapili kutoka kushoto. Picha na Mrisho Sadick

Geita kuondoa vikwazo kwa wakulima ikiwemo kutatua changamoto ya upatikanaji wa mbolea ili kufikia malengo ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa wingi.

Na Mrisho Sadick – Geita

Mkoa wa Geita umekusudia kuzalisha Hekta zaidi ya laki tano za chakula kwa mwaka 2023/2024 ili kukabiliana na Changamoto ya upungufu wa chakula kutokana na mabadiliko ya Hali ya hewa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Mohamed Gombati kwenye kikao cha wadau wa Kilimo Cha kujadili changamoto na mafanikio kwenye sekta hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.

Wadau wa kilimo Mkoani Geita wakiongozwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Geita wapili kutoka kushoto. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Katibu tawala Mkoa wa Geita

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Cornel Magembe amesema Hali ya upatikanaji wa Mbolea Mkoani Geita ni asilimia 28 ambazo nisawa na tani 1,162 huku mahitaji yakiwa ni Tani 4,084 nakuviagiza vyama vikuu vya ushirika kuhakikisha vinasambaza mbolea kwa wakulima.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita