Storm FM
Storm FM
6 June 2026, 9:23 pm

Ujenzi wa ofisi hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha shughuli za CCM ngazi ya kata na kuweka mazingira bora ya utekelezaji wa majukumu ya chama
Na Mrisho Sadick:
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nikolaus Kasendamila amewataka wanachama wa chama hicho kuachana na tofauti zilizojitokeza wakati wa uchaguzi na kuelekeza nguvu zao katika kukijenga chama pamoja na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama.
Akizungumza katika Kijiji cha Ichwankima wilayani Chato wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata hiyo katika ziara yake ya Kata kwa Kata Kasendamila amesema uchaguzi umekwisha na waliokuwa wakigombea nafasi mbalimbali sasa wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya chama.

Katika hatua nyingine Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Reuben Sagayika amechangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa ofisi hiyo huku akitoa wito kwa wanachama na wananchi kuendelea kushiriki katika maendeleo ya chama na jamii inayowazunguka.
