Storm FM

Wajasiriamali wa soko la Lukilini kujengewa vizimba 50

13 April 2024, 3:12 pm

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano ulioitishwa na viongozi wa mtaa huo katika soko la Lukilini. Picha na Kale Chongela

Wafanyabiashara walio wengi hasa wale walioko katika maeneo ya vijijini au nje ya miji hukabiliwa na changamoto ya miundombinu duni ya kufanyia biashara zao

Na Kale Chongela – Geita

Baadhi ya wajasiriamali waliopo soko la Lukilini Mtaa wa Mkoani Kata ya kalangalala Mjini Geita wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe Costantine Kanyasu kwa kutoa fedha ili kuwejengea vizimba katika soko hilo.

Muonekano wa soko la Lukilini Geita mjini. Picha na Kale Chongela

Wakizungumza na Storm Fm wajasiriamali hao wamesema kuwa kukamilika kwa vizimba hivyo itawasadia baadhi yao kuachana na kuuzia chini  na kwamba soko hilo litakuwa na mvuto katika biashara zao tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Sauti za wajasiriamali waliopo soko la Lukilini

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa mkoani ambapo ndipo soko la Lukilini lilipo Bw Salvatory Daniely amesema yupo tayari kusimamia fedha hizo ili zitumike kwenye malengo ambayo yamekusudiwa na si vitu vingine  ili eneo hilo liweze kuwanufaisha wajasiriamli waliopo katika soko la lukilini .

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mkoani

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mtaa wa Mkoani Bw Amos Daudi amesema kuwa jumla ya Fedha ambazo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe Costantine John Kanyasu ni Milioni 30 kwa ajili ya kutengeneza vizimba 50 kwa ajili ya kupanga bidhaa katika soko hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa Tawi la CCM mtaa wa Mkoani
Muonekano wa baadhi ya vizimba vinavyotumiwa na wafanyabiashara katika soko la Lukilini. Picha na Kale Chongela