Storm FM

Watu Wawili Wakamatwa Wakichinja Mbwa Geita

20 May 2021, 2:25 pm

Na Zubeda Handrish:

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu wawili ambao hawajafahamika kwa majina yao wamekamatwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa wakichinja mbwa katika mtaa wa Msalala road Halmashauri ya mji wa Geita.

Wakizungumza na Storm FM wananchi wa mtaa huo wamesikitishwa na kitendo hicho na kuomba watu hao wachukuliwe hatua za kisheria kwa kumchinja myama huyo aina ya mbwa bila ya kufuata taratibu za uchinjaji na kuongeza kuwa, huenda baadhi ya maeneo watu watakuwa wameshalishwa nyama ya mbwa.